Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA-, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Muhammad Baqer Dhu al-Qadr, amesema kuwa mashambulizi endelevu na yaliyoelekezwa yanayofanywa na wapiganaji wa Iran yataendelea hadi adui asalimu amri kikamilifu.
Katika ujumbe aliouandika, Dhu al-Qadr amesema kuwa kila nguzo ya moshi inayoonekana katika eneo hilo ni ishara ya kulengwa kwa kituo cha kijeshi, kiusalama au kifedha cha Marekani.
Amesema mashambulizi hayo yanaendelea katika kipindi ambacho Iran inasisitiza kulipiza kisasi kwa damu za watoto wasio na hatia waliouawa katika maeneo ya Minab na Lamerd, yaliyoko kusini mwa Iran.
Akihitimisha ujumbe wake, Katibu huyo wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa amesema:
“Mashambulizi endelevu na yaliyoelekezwa kwa usahihi yanayofanywa na wapiganaji wetu ni mijeledi ya hasira ya wananchi wa Iran wanaopambana, inayomwangukia mfumo wa utawala wa kibeberu. Mashambulizi hayo yataendelea hadi adui asalimu amri kikamilifu na kulipiza kisasi kwa damu za watoto wasio na hatia wa Minab na Lamerd… kwa uwezo na msaada wa Mwenyezi Mungu.”
Maoni yako